0

Wanaukumbi kwema,

Leo naombeni mnijuze nini kimemkuta mwanamuziki Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ambaye kuna kipindi tuliaminishwa kuwa atakuja kumzidi kama sio kumfunika na kumpoteza kabisa Diamond.

Ikumbukwe Ommy Dimpoz alianza vizuri kwa kutoa vibao matata kama Nainai, Baadae, Tupogo na Ndangushima. Baada ya hapo ametoa nyimbo zilizoshindwa kutamba kabisa...mfano mzuri ni Wanjera. Kwasasa dimpoz amepotea na kafunikwa na vijana wadogo akina Rayvan na Harmonize, Je ni nini kimemsibu staa huyu aliyekuwa anafananishwa na Diamond kwa uwezo wake Kimuziki?

Post a Comment

 
Top