0


Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi. 

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj. 

Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi. 

Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake. 

“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema. 

Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande. 

Mzazi wa Mamba, Fatuma Alli alisema alipata taarifa ya tukio hilo baada ya siku tatu na kwamba, siku hiyo hiyo mume wa mwanamke aliyetenda kitendo hicho alikwenda kwake akieleza kijana huyo alijaribu kumbaka mkewe. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba, alisema hana taarifa za tukio hilo. 

Daktari wa meno wa hospitali hiyo, Dk Hamisi Kakandilo alisema ulimi wa kijana huyo hauwezi kutibika isipokuwa kuusafisha ili asipate maambukizi. 

“Hata kama kipande kilichotolewa kingepatikana kisingeweza kushonwa,”alisema.

Post a Comment

 
Top