0
Shirikisho la wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali  TAMONGSO watoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi kwa kuliagiza Baraza la Taifa la Mitihani kufuta mfumo unaotumika sasa wa Wastani wa Alama (GPA) na kurudi katika mfumo uliokuwa unatumika hapo awali wa division.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Taifa wa TAMONGSO Bwa. Mrinde Mzava amesema kuwa Waziri wa Elimu Ameitendea haki Sekta ya Elimu kwani mfumo huo ulileta sintofahamu kwa wananchi wengi.

Post a Comment

 
Top