Mwanadada asiyeishiwa matukio Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ amenaswa kimalovee na rafiki wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ huku ikidaiwa ni ‘mtu’ wake.
Chanzo makini kililiambia gazeti hili kwamba jamaa huyo ambaye anajiita Dangote Kifyagio ni rafiki wa Diamond ambaye alikuwa akimsaidia mambo yake kimuziki ili awe juu.
wema (3)“Wema yuko karibu sana na huyu jamaa (Dangote), hata Singida alikuwa akizunguka naye sehemu mbalimbali.
Ndiyo maana kuna picha kibao ambazo zinawaonesha wakiwa romantic kiasi kwamba wapo wanaokwenda mbali na kusema ni wapenzi, watu bwana,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Unajua yule Kifyagio alikuwa rafiki wa Diomond sana huko nyuma, sasa isije ikawa kaamua kujiweka kwa shemeji yake maana si unawajua tena hawa mastaa wetu, nyie fuatilieni mtaujua ukweli.”
Baada ya gazeti hili kunasa ‘ubuyu’ huo pamoja na picha za Wema na jamaa huyo wakiwa kimahaba sehemu tofautitofauti, lilimvutia waya mrembo huyo na kumbana kuhusu uhusiano =wake na Dangote Kifyagio ambapo simu yake haikupokelewa.
Alipotumiwa ujumbe juu ya madai kuwa anatembea na jamaa huyo alijibu kwa hasira kama ifuatavyo:
“Halafu sikia nikwambie, vitu vingine ni upuuzi tu hivyo vitu vinaniharibia deal zangu na mipango yangu yote, sipendi hata kidogo, yaani sipendi kwanza kufuatiliwa, amekuwa mtu wangu?
Nishawahi kumposti na kusema ni bwana’angu zaidi ya mimi na yeye kuheshimiana? Nina bwana wangu ambaye ndiye kila kitu kwangu jamani sipendi wallah…sipendi.”
Post a Comment