0

Walinzi wa italia wanasema kuwa takriban wahamiaji 3,000 wako mashakani
Walinzi wa pwani wa Utaliano wanasema kuwa waliaongoza shughuli za kuwaokoa wahamiaji 2,000 hivi ambao walituma ishara ya kuwa taabani kwenye mashua nje ya pwani ya Libya. Mashua kadha zinashiriki katika uokozi.
Mashua kama 18 za raba na mashua nyengine zilizojaa wahamiaji zimetuma ujumbe kwamba ziko mashakani.
Bahari baina ya Libya na Utaliano, ndio njia inayotumiwa kwa muda mrefu, na wakimbizi kutoka Afrika na Mashariki ya Kati, ili kuingia Ulaya.
Kati ya wahamiaji 264,500 Umoja wa mataifa unasema kuwa bahari ya Mediterranea ndio kivukio maarufu.

Kufikia sasa takriban watu laki moja wamewasili katika ufukwe wa Italia .
Manuari ya Kijeshi ya Norway ilikuwa imewaokoa wahamiaji 320 jumamosi asubuhi


Post a Comment

 
Top