0
BUSU walilopigana mrembo wa Bongo Movies, Wema Sepetu ‘Madam’ na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba lilizua gumzo la aina yake huku wambea wakisema; “wamependezana.”

‘Katukio’ hako ka’aina yake kalitokea wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar kulipokuwa na hafla ya umoja wa wasanii waliokuwa wakimuaga Rais Jakaya Kikwete, anayemaliza madaraka yake, Oktoba 25, mwaka huu.

Wakati shamrashamra zikiendelea, muda wa kucheza muziki, Madam alikutana uso kwa uso na Makamba ambaye anapenda kucheka na kila mtu, wakakumbatiana na kubusiana ‘kiaina’ hali ambayo iliwafurahisha watu wengi.
“Wamependezana. Makamba mtu poa, imenishtua kidogo walipochelewa kuachiana lakini najua ni salamu ya kumisiana tu,” alisikika shuhuda mmoja.
Wawili hao kila mmoja ana mtu wake, kukumbatiana huko na kubusiana kulikuwa ni kwa Kawaida tu

Post a Comment

 
Top