0
Kwa taarifa zilizotufikia leo kutoka Mkoani Arusha zinasema kuwa aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani Mh.Lawrence Masha kakihama Chama cha Mapinduzi na kujiunga na CHADEMA leo.Pia Wanachama wa (CCM) na viongozi ambao ni Daniel Porokwa aliyekuwa katibu wa CCM mkoani Manyara, Robinson aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Arusha, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa Arusha, Goodluck Sipira aliyekuwa katibu wa CCM mkoani  Arusha huyu anatokea Longido, aliyewahi kuwa mgombea Ubunge kupitia CCM pale Arumeru Mashariki ndugu Sioi Sumari, Wazee wa Kimila wa Kimasai  pamoja na Wazee wa kimila wa Kimeru wote wakiongozwa na Mshili Mkuu leo wamejiunga rasmi kwenye chama cha CHADEMA

Post a Comment

 
Top