0
Joseph Haule 'Prof. Jay' akiionyesha kadi aliyokabidhiwa kwa kujiunga na CHADEMA akiwa na Wabunge wa chama hicho, Josepj Mbilinyi 'Sugu' na John MnyikaMTANGAZA nia ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi ya kugombea ubunge katika jimbo la Mikumi na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jimboni humo, Onesmo Mwakyambo,  ametangaza kujiengua katika chama hicho na kujiunga na ‘Alliance for Change and Transparency-ACT Wazalendo, kwa madai ya kutukanwa na kudhalilishwa.
Akizungumza na Mwanahalisi Online, Mwakyambo alikiri kukihama Chadema na Kujiunga na ACT Wazalendo, katika Mkutano uliofanywa na Katibu wa Kamati ya Maadili ya ACT-Wazalendo Taifa, Gibson Kachingwe.
Hata hivyo, Mwakyambo alipata wakati mgumu pale alipojikuta akizomewa na nguvu ya umma kabla hajapanda jukwaani, na hata aliposhuka  huku akisindikizwa na nyimbo za kumzomea kuwa ni msaliti, kama yuda  Eskariote. 
“Ni kweli Mwandishi nimejiunga ACT-Wazalendo, kwa muda mrefu nimevumilia kutukanwa, kudhalilishwa, na mbaya zaidi, nimeandikiwa ripoti mbaya kuhusiana na mgogoro wa uhusiano wa uongozi wa Kata ya Ruaha na Kijiji hicho, hivyo ni bora nipumzike, nitahamishia majeshi huko. 
”Nimemwarifu Katibu wa Chadema Mkoa, Samuel Kitwika, akate fomu  yangu niliyowasilisha kwa utia nia wa ubunge wa Chadema  Jimbo la Mikumi, na badala yake nataka kuhamishia nia yangu ACT-Wazalendo, lakini ninachokiona, nafanyiwa rafu, amesema Mwakyambo. 
Kitwika alikanusha kwamba, Ofisi ya Chadema Mkoa wa Morogoro ina madudu na upendeleo na kusema, “mko tunafanya kazi zetu kwa kufuata Katiba ya Chadema, Sheria na Taratibu zilizoweka, makandokando yake na kubanwa kwake jimboni, asihamishie kwetu”.amesema
Mbali ya Kitwika kukiri Mwakyambo kukihama Chadema, alikanusha taarifa kuwa alikuwa anatukanwa, kudhalilishwa na kuandikiwa ripoti mbaya bila kumtaja aliyemtuka, ila akasema,  Chadema Mkoa kupitia Intelijensia yake, ilikuwa na taarifa za mienendo yake mibaya ya Mwakyambo dhidi ya Chadema, ikiwemo la kuhamia ACT-Wazalendo. 
“Huyu ni Msaliti, tulimshitukia siku nyingi,tukakosa imani naye, hana madhara yoyote kwa Chadema, tuko imara, na ndiyo maana tumemzomea sana kwa kwenda mbele, tangu alipokuwa jukwaani hadi aliposhuka kuelekea kwake,” amesema Mwilenga.

Post a Comment

 
Top