Msanii wa muziki Kala Jeremiah amewataka wasanii wenzake kufanya nyimbo za kijamii bila kuogopa kama zitafanya vizuri.
Akiongea na Bongo5 Jumatato hii, Kala amewataka wasanii kuacha kuogopa kufanya muziki wa kijamii kwa hofu ya kutofanya vizuri.
“Mimi ningewaambia wasanii wenzangu nyimbo za kijamii ndio nyimbo ambazo zinafanya vizuri bila taka kuumiza kichwa, nyimbo za kijamii zinalipa sana tofauti na wasanii wanavyofikiria, mimi nina wimbo wangu ‘Wanandoto’ umefanya vizuri sana, tena naweza kusimama jukwaani na msanii mwingine lakini mimi nikala shangwe la kufa mtu.Kwa hiyo mimi nawashauri tu, tuzikumbuke jamii tunazotoka,” alisema Kala.
Rapper huyo amesema wimbo ‘Wanandoto’ unampatia deal nyingi kubwa za kijamii tofauti na baadhi ya wasanii wanavyofikiria
Post a Comment