0

WIZARA ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.

Mpango amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa  pamoja na waliokwepa kodi  yashughulilikiwe.

Ahadi ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya  kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha za maendeleo  katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.

Post a Comment

 
Top