Muimbaji wa R&B, Jux ambaye video yake mpya ‘Looking For You’ imetambulishwa kwa mara ya kwanza August 11 kupitia MTV Base, amesema kuwa nafasi hiyo hakuipata kwa sababu ya Vanessa.
Licha ya kuwa Vanessa Mdee ambaye ni girlfriend wake kufanya kazi na MTV kama VJ, lakini video yake haikupewa nafasi kwa sababu hiyo.
“Vanessa yeye ni msanii kama mimi..ingekuwa hivyo basi kila video yangu ingekuwa inapigwa MTV.”Jux alisema kupita 255 ya XXL.
“Kila video yangu nilikua najaribu kutuma MTV lakini kulikuwa na vitu ambavyo tulikuwa tunapishana, sijui wao walikuwa wanaangalia vigezo gani. Lakini nimepata bahati video yangu niliyofanya sasa hivi imekubaliwa.”
Kabla ya ‘Looking For You’ Jux aliwahi kutuma video tatu ambazo zote hazikuchezwa na MTV.
“Video kama Tatu, ambayo ilikuwa Siikii, Nitasubiri walikaa tu kimya nilituma lakini sikupata majibu yoyote lakini nilipotuma hii walijibu wakasema sawa tutakupa siku flani tarehe.”

Post a Comment