Unaweza ukaanza kujizoesha kumuita kwa jina lake jipya, Mheshimiwa Irene Uwoya kwasababu mrembo huyo amepita kwenye kinyang’anyiro cha viti maalum vijana taifa.
Kupitia mkutano wa halmashauri kuu ya CCM uliofanyika mjini Dodoma kuanzia juzi, Uwoya amepata kura nyingi za kumwezesha kuingia mjengoni mwaka huu.
Akiongea na XXL ya Clouds FM, Uwoya amesema awali katika kura hizo alifungana na mtu mwingine na hivyo ukafanyika uamuzi wa kumchagua mmoja.
“Niliweka mtu wa kunihesabia kura lakini tukafungana, tukajikuta watu wawili tumefungana lakini baadaye hatukutangaziwa majibu kwasababu kamati zilikuwa hazijakaa kuamua kwahiyo sasa hivi ndio nimepata majibu,” amesema.
“Tabora nilipita kwa kura nyingi sana na huku taifa pia nimepita kwahiyo namshukuru Mungu.”
Krish akiwa na mama yake Mheshimiwa Irene Uwoya
Naye mume wake, Hamadi Ndikumana ametumia mtandao wa Instagram kumpongeza mke wake kwa kuukwaa ubunge.
“Hongera sana mke wangu kwa ushindi uloupata,tumshukuru Mungu kwa kupokea maombi yetu na kukufikisha ulipo stahili.Kama nnavyo kwambia siku zote binadamu hukupenda pale wanapoona watapata faida wapo wengi ulikua nao karibu wengine uliwasaidia mda mrefu ila wakati uliwahitaji walijitenga nawe,” ameandika.
“Kwangu ni faraja kubwa na naona kama Mungu alipanga hivyo kurejesha furaha ya penzi na ndoa yetu,siku chache tu zimepita nikirudi uwanjani baada mda mrefu pia kupata nafasi yakuwa karibu na familia yangu.Namshukuru Mungu kwa kunirejesha karibu na familia yangu tena kwa kishindo kikubwa.Mungu azidi kukusimamia na akuongoze kataka nafasi hiyo mpya aliyo kupa muheshimiwa mbunge viti maalum kupitia chama chako cha ccm.”

Post a Comment