0
Hussein Machozi amedai kuwa wakati anafikiria kufanya kazi na kundi la muziki la nchini Kenya la Sauti Sol, alidhani lingemletea mapozi.

Akiongea na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Machozi amesema aligundua kuwa wasanii hao ni watu wa watu.

“Yaani kabla ya kuthubutu na kuwatafuta Sauti Sol kwaajili ya kufanya nao kazi, nilidhani huenda jamaa watakuwa wagumu kukubaliana na ombi langu. Lakini mambo yalikuwa tofauti na vile nilivyokuwa nafikiria,” amesema Machozi.

“Unajua mwanzo nilikuwa naamini ni vigumu sana kufanya kazi na Sauti Sol, lakini kila kitu ni kujaribu. Niliwafuata na kuwaeleza nahitaji kufanyakazi na nyinyi na wakakubali bila kipingamizi chochote. Nilishangaa pia kujua kumbe hata Sauti Sol wanakubali kazi zangu,” ameongeza.

“Kazi hiyo ilifanyika ingawa iliniwia ugumu sana kutengeneza wimbo huo kwa sababu ya kupishana kwa muda wa kufika studio, jambo ambalo liliwafanya kutumia wiki nzima mpaka wanakamilisha wimbo huo wa ‘Utapenda’ ambao ulirekodiwa nchini Kenya.”

Post a Comment

 
Top