kwa mwaka 2015-2020, ikitaja mambo makuu manne ya kushughulkikia katika miaka mitano ijayo, ambayo ni kupambana na umaskini, ajira kwa vijana, ulinzi na usalama na kupambana na rushwa kwa kuanzisha mahakama maalumu ya makosa hayo.
Ilani hiyo, iliyoandaliwa na makada wake 32 wakiongozwa na Stephen Wasira, imeanisha jinsi chama hicho kikongwe kilivyotekeleza baadhi ya ahadi zake katika ilani ya mwaka 2010-2015 na kutaja ahadi mpya zikiwamo zinazohusu ujenzi wa miundombinu, kukuza uchumi, viwanda, nishati, kilimo, sanaa na michezo pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.“Ilani hii ni tamko maalumu kwa wapigakura kuhusu nia ya CCM ya kuendelea kushika dola na kuwaongoza Watanzania kwa njia ya kidemokrasia na hasa kuendelea kudumisha amani, umoja wa kitaifa, usawa, ustawi wa wananchi, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa kipindi kingine cha miaka mitano,” inasema ilani hiyo.Kukamilika kwa ilani hiyo sasa kutamuweka huru mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli ambaye amekuwa akisita kumwaga sera kwenye mikutano ya hadhara kwa hofu ya kukiuka Sheria ya Uchaguzi na pia kutokuwapo kwa ilani hiyo.Mkutano Mkuu wa CCM ulikuwa upitishe ilani hiyo Julai 12 mjini Dodoma, lakini mwenyekiti wa chama hicho, Jakaya Kikwete akaeleza kuwa ilikuwa katika hatua za mwisho za uhariri na kuomba chombo hicho kiridhie kazi hiyo kukamilishwa na Halmashauri Kuu.Kwa mujibu wa ilani hiyo yenye kurasa 236, katika miaka mitano ijayo CCM itazielekeza Serikali zake za Muungano na Zanzibar kuboresha maisha ya wananchi wote na hususan vijijini, kwa kuchukua hatua mbalimbali ilizoziainisha, zikiwamo kukuza kilimo, miundombinu, viwanda, ajira na kupambana na rushwa.Katika suala la rushwa, ilani hiyo imetaja mkakati wa mmoja wa makada walioomba kuwania urais kwa tiketi ya chama hicho, Frederick Sumaye wa kuanzisha mahakama maalumu ya kushughulikia matatizo ya rushwa.Ilani hiyo inaeleza kuwa CCM itaimarisha “vyombo na taasisi zinazohusika katika kuzuia na kupambana na rushwa, ikiwa ni pamoja na kuanzisha mahakama maalumu kwa ajili ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi”.Mkakati huo umekuja wakati chama hicho kikikabiliwa na tuhuma za rushwa, hasa katika mchakato wa uchaguzi huku makada wake wakihusika katika kashfa zilizotikisa Taifa, hasa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyosababisha mawaziri wawili kuachia ngazi, sambamba na Mwanasheria Mkuu, wabunge na baadhi ya watendaji waandamizi wa Serikali.CCM inaeleza katika ilani hiyo kuwa imedhamiria kukuza uchumi kwa miaka mitano ijayo kwa wastani wa asilimia nane au zaidi, kuinua ustawi wa Watanzania kwa kuongeza mapato ya wananchi kufikia kiwango cha wastani wa nchi ya uchumi wa kati, hivyo kuongeza fursa za ajira na kupunguza umaskini.Ahadi nyingine katika kukuza uchumi ni pamoja na kudhibiti mfumuko wa bei uendelee kubaki kwenye tarakimu moja, kudhibiti nakisi ya bajeti ili iendelee kushuka na kufikia kiwango kisichozidi asilimia tatu ya Pato la Taifa, pamoja na mambo mengine, Tanzania iendelee kupunguza gharama za kukopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi.Katika miundombinu, CCM imeendeleza ahadi za kujenga barabara, madaraja, vivuko, viwanja vya ndege, nyumba na majengo ya Serikali ili kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii.Hata hivyo, msisitizo wa ujenzi wa barabara umewekwa zaidi katika zile zinazounganisha Tanzania na nchi jirani, mikoa, na barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi kama Mchuchuma na Liganga na kujenga madaraja mapya ya Selander jijini hapa na Wami Chini la mkoani Pwani.CCM imekusudia kuhamasisha kilimo kupitia kaulimbiu ya Kilimo Kwanza, kwa kuwawezesha wakulima kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa, pembejeo, zana za kisasa na wataalamu wa ugani pamoja na mbinu za kuyafikia masoko ya uhakika ya mazao yao.CCM inakusudia kuongeza kasi ya kupima ardhi na kuwapatia hatimiliki za kimila wananchi, ambazo watazitumia kama dhamana ya kuwawezesha kupata mikopo ya kuendeleza shughuli mbalimbali za kilimo, ufugaji na uvuvi.“Kuendeleza na kuimarisha huduma za kijamii ikiwamo elimu, afya, maji, umeme na ujenzi wa nyumba bora pamoja na kuongeza kasi ya kurasimisha biashara kwa kuwapatia wafanyabiashara wadogo maeneo ya kufanyia biashara, leseni na fursa za kupata mikopo yenye masharti nafuu,” ilani hiyo inaeleza.“Kuanza na kukamilisha ujenzi wa viwanja vya ndege vya Shinyanga, na Sumbawanga kwa kukarabati barabara za kutua na kuruka ndege, kujenga na kukamilisha awamu ya pili viwanja vya Tabora na Kigoma na kuanza ujenzi wa kiwanja cha Ndege cha Msalato kwa kiwango cha kimataifa,” inasema ilani hiyo.Katika sekta ya afya, CCM imeahidi masuala mbalimbali ikiwamo kujenga hospitali tatu za rufaa kwa Kanda za Kusini, Kati na Magharibi na kuendelea kuimarisha zilizopo.Iwapo itapatiwa ridhaa ya kushika dola, CCM imepanga kudahili wanafunzi 15,000 katika vyuo vya afya ifikapo 2020 kama jitihada kutosheleza mahitaji ya rasilimali watu na kuajiri wataalamu zaidi wa afya kutoka ndani na nje ya nchi kuboresha huduma za afya.Ahadi nyingine ni kuimarisha upatikanaji wa dawa, huduma za mama na mtoto, kuimarisha huduma za matibabu ikiwamo kununua mashine za mionzi kwa ajili ya saratani na kuweka utaratibu wa wananchi kupata Bima ya Afya.Kwa kutambua umuhimu wa ukuaji wa sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia, CCM imeahidi kutenga kila mwaka kiasi kisichopungua asilimia moja ya pato ghafi la Taifa (GDP), kwa ajili ya utafiti, maendeleo na maonyesho.Pia, kuwalinda watumiaji wa simu za mikononi dhidi ya uhalifu wa mitandaoni na kuongeza watumiaji wa intaneti kutoka milioni tisa mwaka huu hadi kufikia milioni 20 mwaka 2020.Wakati baadhi ya wakosoaji wa masuala ya elimu wakieleza kuwa ubora wa elimu unapungua, CCM imekusudia kuhakikisha uandikishwaji wa rika lengwa la wanafunzi wa kidato cha kwanza unaongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2015 hadi asilimia 80 mwaka 2020... “Ufaulu wa mtihani wa kidato cha nne utaongezeka kutoka wastani wa asilimia 69.8 mwaka 2015 hadi asilimia 90.0 mwaka 2020 na ufaulu wa daraja l hadi lll kutoa wastani wa asilimia 30.8 hadi asilimia 50.0.”

Post a Comment