0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetangaza siku ya urejeshaji fomu za Urais na Makamu wa rais kuwa ni Alhamis ijayo.

Aidha, imepiga marufuku maandamano na badala yake watu saba tu ndio wataruhusiwa kusindikiza wagombea.

Taarifa ya Nec kwa vyombo vya habari jana na kusainiwa na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima, ilisema urejeshaji fomu utaanza saa 1:30 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

Alisema wagombea wote wanatakiwa kufika kwenye ofisi za Tume wakisindikizwa na watu hao na majina yao yawasilishwe Tume kabla ya Agosti 20, ili kuratibu kazi hiyo.

"Wagombea hawaruhusiwi kuja Tume kwa maandamano, shamrashamra, nderemo wala vifijo. Hii ni kwa sababu siku hiyo vyama vya siasa vitakavyowasilisha fomu za kuomba uteuzi vitakuwa vingi hivyo kila chama kikija Tume kwa maandamano na shamrashamra kunaweza kutokea uvujifu wa amani," alisema.

Alisema sababu nyingine ni kuwawezesha wananchi wengine kuendelea na shughuli zao na sababu ya tatu ni kuimarisha amani na utulivu na kwamba ni vyem vyama vikafuata maelekezo hayo.

Post a Comment

 
Top