0


Serikali ya Tanzania imesema kwamba kulingana na takwimu inaonesha kuwa  ukosefu wa ajira kwa vijana nchini Tanzania umepungua kwa asilimia mbili, kutoka asilimia 13.7 mwaka 2012 mpaka asilimia 11.7 mwaka huu.

Akizungumza jana bungeni, mjini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu Mhe. Anthony Mavunde,  alisema licha ya kupungua huko kwa ukosefu wa ajira, serikali imeweka mipango ya kuwawezesha vijana kuwa na wigo mpana wa ajira nchini.

Mhe. Mavunde alisema kuwa kwa takwimu hizo Tanzania ni nchi inayoongoza kwa kutoa ajira kwa vijana wengi zaidi kushinda baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda.

Post a Comment

 
Top