Messi ambaye saivi ana umri wa miaka 29 aliifungia Barcelona bao la kwanza katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Sevilla.
Messi ameifungia Barca mabao 500 katika mechi 592,ikiwemo mechi za kirafiki huku mechi 469 zikiwa rasmi.
Messi sasa anakuwa amemshinda aliyekuwa na mabao mengi Paulino Alcantara ambaye aliichezea Barcelona katika vipindi viwili vya kati ya 1912 na 1927.
Mnamo mwezi Aprili,mshambuliaji huyo alifunga bao la 500,ikiwemo mechi za kimataifa,wakati Barcelona iliposhindwa 2-1 na Valencia.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.