Kumfanya mwanaume aweze kuwa na majukumu ya kimaisha ni
vigumu, lakini hizi mbinu ambazo tuko nazo za kumfanya mwanaume akuoe
zitahakikisha umesimama na yeye madhabahuni haraka sana.
Hivi wewe umekuwa katika mahusiano na mwanaume kwa muda
mrefu mpaka unaanza kushuku iwapo huyu mwanaume yuko serious na wewe ama
anakuchezea tu? Na umekuwa kila siku ukimwomba Mola akusaidie angalau amfanye
huyu mwanaume ulie naye atoe ishara za kuwa atakuoa mbeleni>
Well, sote tunajua kuwa ndoto ya kila mwanamke ni kuwa siku
moja katika maisha yake atakuja kuolewa kwa harusi...so sisi hapa tunataka
kukupa maujanja ya kumfanya huyo mwanaume atake kukuoa haraka sana.
Zama nasi...
#1 Kuwa girlfriend kamili. Hivi wewe na mwanaume huyu mumekuwa na maisha ya fanaka. Nyote
wawili mumeinjoy maisha ya furaha, mumezama katika mapenzi, na unaona kwamba
una uwezo wa kumwambia kila kitu ambacho unakifikiria. Lakini hebu ngoja kidogo
na ufikirie mambo ambayo unaweza kufanya zaidi ya hayo.
Mfanye ajihisi kuwa anakubalika, yuko salama na special,
haya ndio mambo ambayo anahitaji zaidi. Bila shaka utakuwa unamjua zaidi ya mtu
yeyote yule. Kile ambacho anapenda na kuchukia, na mambo ambayo yatamfanya
akuone kuwa wewe unapendeza zaidi ya kitu chochote kile.
Hakikisha unafanya kila kitu ambacho mwanamke kamili anaweza
kufanya. Mwonyeshe kila kitu ambacho anahitaki, na bila shaka atakuona wewe
umejitweka jukumu la kuhakikisha kuwa wewe uko hapo kwa ajili yake.
#2 Mtunze. Kama
mwanaume anahisi kuwa hawezi kuishi bila wewe, basi bila shaka atahakikisha ametia
kufuli jambo hilo.
Hakikisha kuwa unamtunza na unamfanya akutegemee kwa mambo
madogo madogo, hata kama ni jambo rahisi lile la kushughulikia nguo zake ama
kumpa sapoti wakati anapohitaji. Wewe kuwa ubavuni mwake kutafanya mabadiliko
ya haraka sana, na hatoweza kustahimili kuishi bila wewe.
#3 Kuwa shabiki wake
mkuu. Jeuka shabiki mkuu wa mwanaume wako. Kitu chochote kile ambacho
ayaamua kufanya, hata kama ni jambo la utani ama la kuchekesha wewe mpe sapoti
kwa kumshabikia atimize azma yake.
Ile siku ambayo atakuja kugundua kuwa mafanikio yake katika
azma yake yamechangiwa na wewe basi atakuweka karibu yake. Atakuona kuwa wewe
umekuwa karibu yake bila hata kupoteza imani katika azma yake. Well utakuwa
umetoboa.
#4 Mtreat. Wakati
mwingine wanaume huchoka kwa kuwa wao ndio kila wakati huwatoa wanawake out na
deti. Msaprize siku moja kwa kumtoa out siku moja, na kuhakikisha unafanya
mambo ambayo anapenda kufanya.
Tumpeleka sehemu romantik, kumtoa katika dinner na
kumuonyesha jinsi romance inavyokuwa kutamfanya achangamke na labda anaweza
ingiwa na jazma ya kukutamkia lile neno ambalo umekuwa ukilingojea kutoka kwake
kwa miaka.
#5 Kuwa mkweli kwa
kile unachotaka. Wanaume wengi si wajuzi wa kusoma akili ya mtu. Wakati
mwingine unaweza kuwa katika mahusiano na mwanaume kwa miaka mingi na
ukashangaa ni kwa nini mwanaume kama huyu hajakuposa. Kuna uhakika mkuu ni kuwa
wazo kama hilo bado halijamlenga kwa kichwa chake.
Kama umekuwa na maongezi ya ukweli na mwanaume wako, na
ukaweka wazi kuwa unampenda, na ukaeleza vile ambavyo unaona mahusiano yenu
yatakuwa miaka inayokuja, basi anaweza kuingiwa na hali ya kutaka kuchukua
hatua ya mbele kuhusiana na unavyosema. Hata kama hana uhakika na ndoa, atleast
utakuwa umeliweka wazo hili katika kichwa chake.
#6 Usikuwe
comfortable sanaa. Kuwa comfortable sana katika mahusiano ni hatari sana.
Haswa iwapo kama unataka mwanaume wako achukue hatua ya mbele. Ni rahisi
kujisahau katika hali ulioko wakati huo na mwishowe kuwa mvivu. La kufanya ni
kuhakikisha kuwa unatafuta maisha yako wewe mwenyewe, interests zako na
marafiki wa kwako.
Hakuna kitu kizuri zaidi kama mwanamke ambaye ana uwezo wa
kujitegemea mwenyewe. Mfanye akuone kuwa wewe una mambo yako ambayo unafanya,
na kuwa una maisha yako ya nje kando na kuwa katika mahusiano. Soon ataanza
kuona jinsi ilivyo rahisi kwako kuenda zako, na hivyo atahakikisha ya kuwa
jambo kama hilo halitokezei.
#7 Usimuogopeshe. Usimuogopeshe
mwanaume ili akupose kwa kuwa hilo si jambo la kufuata. Inakubalika kuongea
maswala ya ndoa, na kueleza msimamo wako. Lakini iwapo utakuwa kila wakati
unamtia presha, kila wakati unagusia swala la ndoa, ama kuanza kutokwa na
machozi kila upitapo mbele ya duka la harusi basi utafanya ile dhana ya kwake
kukuoa kufifia haraka sana kwani atakuogopa.
#8 Mwonyeshe kuwa
wewe ni wife material anayemwota. Ukimwona mwanaume ameamua kuwa wewe ndie
aliyekuchagua basi tayari alikuwa alikuweka kwa ndoto zake awali.
Kama unamtaka aweke pete kwa kidole chako, basi mwonyeshe
kuwa wewe utakuwa mke mwema. Kuwa mtiifu, mwaminifu, mpole, mvumilivu, na
mpendezi. Muda si mrefu ataona kuwa hakuna mwanamke yeyote ambaye anaweza
kuzishinda tabia ambazo uko nazo.
#9 Rudi nyuma. Kama
imepita muda mrefu na umeshajaribu mbinu zote tulizozitaja hapo juu, basi jambo
la mwisho ambalo unaweza kufanya ni kurudi nyuma kiasi. Kumpatia mwanaume wako
nafasi ya kupumua si jambo baya, Si lazima ufanye mambo mazito ya kuleta
atenshen ya bure. Kwa kupoa kiasi, anaweza kuhisi kutokuwepi kwako na kugundua
kuwa maisha yatakuwa hayana maana kama hautakuwa na yeye.
Atagundua kuwa maisha yake ni mahumu bila wewe na hapo hapo
atakutaka uwe na wewe zaidi kuliko awali.
Post a Comment