0
Beyonce amechukua siku chache ya kumpumzisha sauti yake na kuahirisha tamasha lake la New Jersey  baada ya madaktari kumshauri afanye hivyo.
487073448_beyonce-zoom-667eecfa-febc-468a-8af7-a22c7b0bc8d1
Queen Bey amefuta show ya Sept. 7 kwenye uwanja wa mpira wa MetLife mjini New Jersey mpaka Oct. 7 baada ya daktari kumuambia apumzishe sauti yake kwanza ili kuendelea na ziara hii.
Ataendelea na tamasha hilo katika miji ya Los Angeles,Houston,New Orleans na Atlanta kama ilivyopangwa.
Ziara hiyo ambayo inalenga kuuza albamu yake mpya Lemonade,ilianza mjini Miami mnamo tarehe 27 mwezi Aprili.
Tour hiyo inatarajiwa kukamilika Nashvile mnamo tarehe 2 mwezi Oktoba,lakini sasa inaonekana kwamba New Jersey ndio itaanda tamasha lake la mwisho.

Post a Comment

 
Top