0
Mgombea mwenza Wa chama cha mapinduzi (CCM) akipokea kadi za chadema kutoka Wa wananchi waliojiunga na CCM
MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu amesema Serikali itakayoundwa na chama hicho endapo itashika dola katika Uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2015 itahakikisha inapima ardhi yote ya vijiji pamoja na kuainisha mipaka ili kukomesha migogoro ya ardhi.


 Bi. Suluhu ametoa kauli hiyo alipokuwa akinadi ilaya ya CCM katika Majimbo mawili tofauti ya Kongwa na Chilonwa Mkoa wa Dodoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake za kufanya kampeni kuwashawishi Watanzania waweze kuipa ridhaa tena Chama Cha Mapinduzi ili kiunde Serikali na kuwatyumikia wananchi.


 Mgombea huyo mwenza wa urais akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Chilonwa Kijiji cha Nzali alisema Serikali ya CCM kwa kushirikiana na halmashauri itaipima ardha ya vijiji na kuweka mipata hasa maeneo sugu ya migogoro kama Kongwa na Kiteto ili kuzuia migogoro na mapigano kwa jamii hizo mbili.
posted from Bloggeroid

Post a Comment

 
Top