0
Mnamo Tarehe 14.08.2015 Mgombea Urais Kwa Tiketi Ya Chadema Alikuja Mkoa Wa Mbeya Akiwa Ameandamana Na Viongozi Wa Vyama Vya Cuf, Nccr – Mageuzi Na Nld Kwa Dhumuni La Kumtambulisha Na Kuomba Udhamini Wa Kupeperusha Bendera Ya Chadema Kwa Nafasi Ya Urais.
Katika Msafara Wake Kutoka Uwanja Wa Ndege [songwe] Kulionekana Gari Moja (pichani) Aina Ya Land Cruiser – Pick Up Yenye Rangi Nyeusi Na Ndani Yake Lilikuwa Limebeba Vijana Ambao Walikuwa Wamevaa Mavazi Meusi, Kofia – Bereti Nyeusi Na Miwani Nyeusi Na Mabuti. 
Watu Hao Walikuwa Na Muonekano Kama Askari Na Shughuli  Waliyokuwa Wakifanya Ya Kuongoza Msafara, Ulinzi Na Kazi Nyingine Zifanyazo Na Jeshi La Polisi.
 
Kutokana Na Muonekano Wao Na Shughuli Walizokuwa Wakizifanya Ilikuwa Ikitafsirika Kuwa Ni Jeshi Lifanyazo Kazi Hizo Ambalo Halikuwa Likifahamika.
Kutokana Na Sintofahamu Hiyo Wananchi Wengi Walikuwa Wakihoji “hilo Ni Jeshi Gani” Sambamba Na Kutuma Picha Kwa Njia Ya Mtandao Wa Kijamii [whatsapp] Wakionyesha Wasiwasi Waliokuwa Nao Dhidi Ya Kikundi Hicho.
Kufuatia Hali Hiyo, Ofisi Ya Mkuu Wa Upelelezi Wa Makosa Ya Jinai Mkoa Wa Mbeya Ilifungua Jalada La Uchunguzi Ili Kuwapata Vijana Wale Kwa Lengo La Kuwahoji Na Kukamilisha Upelelezi Ili Jalada Lipelekwe Kwa Mwanasheria Wa Serikali Kwa Ufafanuzi Wa Kisheria.
Hii Ni Kutokana Na Kuibuka Kwa Makundi Ya Aina Hii Hasa Kwa Vyama Vikubwa Vya Siasa Hapa Nchini.
Katika Kufanya Ufuatiliaji Huo, Wapo Watu Wawili Walikamatwa Alfajiri Ya Leo Tarehe 18.08.2015 Kwa Mahojiano Na Baada Ya Maelezo Yao Kuchukuliwa Walipewa Dhamana. 
Baadhi Ya Viongozi Wao Waliokuja Polisi Wameelezwa Kuhitajika Kwa Vijana Wale Waliokuwa Katika Gari Lile Ili Wahojiwe Na Kukamilisha Upelelezi Wa Jalada Hilo Mapema Ili Mwanasheria Wa Serikali Alitolee Mwongozo Wa Kisheria.
 
           Imesainiwa Na:
[ahmed Z. Msangi – Sacp]
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya

Post a Comment

 
Top