0
Mwanafunzi wa kidato cha pili wa Sekondari ya Nyasubi, Ally Jacob ameuawa baada kuchomwa na kitu chenye ncha kali shingoni alipokuwa akijaribu kumwokoa mwanafunzi mwenzake asibakwe.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 9:00 alasiri maeneo ya Nyasubi, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. alikuwa akirejea nyumbani kutokea shuleni.

Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Justus Kamugisha alidai kuwa mwanafunzi huyo aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya shingoni na mwenzake anayesoma Sekondari ya Kishimba.

Kamugisha alisema sababu za Jacob kuuawa ni kujaribu kumsaidia mwanafunzi mwenzake mwenye umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa) ambaye anasoma kidato cha pili Sekondari ya Nyasubi ili asibakwe na mtuhumiwa ambaye alitaka kufanya unyama huo kwa kushirikiana na mkazi mmoja wa Nyasubi.

Alisema watuhumiwa wote wamekamatwa na watafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Post a Comment

 
Top