0
Wakati jina la Latifah mtoto wa Diamond na Zari likizidi kukuwa, rafiki wa karibu wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Ssemwanga, Kinglawrence amemtupia dongo Diamond akisema hakuhitajiki kipimo chochote cha vinasaba DNA ili kujua kuwa, Latifah si mtoto wa Diamond kwani mambo yamejionesha yenyewe baada ya miezi tisa.
Kwenye mtandao wa Instagram, jamaa huyo aliweka picha ya Ivan aliyoiunganisha na picha ya Latifah ili wadau waone walivyofanana. Hapa ana maana kuwa, mtoto huyo ni wa Ivan.

Diamond alipotafutwa aseme neno kuhusiana na madai hayo yote, alipuuza kuhusu mtoto ni wake au si wake, akasema ana furaha iliyopitiliza ya kupata mtoto na kuhusu jina haoni kama kuna tatizo.

Post a Comment

 
Top