Mwimbaji nyota wa nyimbo za Injili, Rose Muhando. | Brighton Masalu |
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Rose alikiri kuingia baadhi ya mikataba na kushindwa kuitekeleza, akisema ni jambo lililomkosesha sana raha, hasa pale watu walipokuwa wakimchukulia kama tapeli.
“Hata hivyo, mara nyingi huwa nasingiziwa, lakini nakaa kimya kwa sababu nimeumbwa hivyo, kama kuna yeyote nimemdhulumu naomba anisamehe, sikufanya makusudi, nilishindwa kutokea kwa bahati mbaya, mimi ni binadamu. Namuomba pia baba yangu mlezi Msama (Alex, Meneja wake) naye kama kuna mahali nilimkwaza kwa matamshi au matendo, naomba anisamehe,” alisema nyota huyo wa kibao cha Facebook.
Post a Comment