0
Habari kuhusu ujio wa collabo kati ya superstar wa Nigeria, Davido na superstar wa Tanzania Alikiba tuliisikia kutoka kwa Davido mwenyewe wakati wa tuzo za 2015 MTV MAMA zilizotolewa huko Durban, Afrika Kusini.

Hatimaye Alikiba naye amezungumzia collabo hiyo kwa mara ya kwanza, kwa kuthibitisha kuwa alichokisema Davido ni kweli hivyo watu wajiandae kupokea kazi hiyo hivi karibuni.

“Davido ameongea na Millardayo kwamba anataka kuja kufanya featuring na Alikiba, which is tayari tulikuwa tumeshaongea muda mrefu, kwahiyo watu wasubirie tu ngoma inakuja kutoka lini.” Alisema King Kiba kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

Alikiba pia ameelezea kile ambacho wanatarajia kukiimba katika wimbo huo ambao bado haujarekodiwa.

“Track iko vizuri, lakini idea bado haijakamilika, lakini kiukweli mi hua nafanya ngoma nikiwa studio, tutazungumzia kuhusu goodtime, party, mapenzi flani you know, yaani nyimbo flani ya kuhamaishisha watu katika raha.”

Post a Comment

 
Top