0

Licha ya serikali kuweka sera ya ushiriki wa makampuni ya kitanzania  katika sekta ya mafuta na gesi bado hayataweza kushiriki katika sekta hiyo kutokana na tatizo kubwa la mitaji itakayoweza kumudu ushindani wa kimataifa katika zabuni zitakazotolewa katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika semina fursa zinazopatikana kwenye msimamizi wa maswala ya ushiriki katika sekta ya mafuta na gesi kutoka wizara ya nishati na madini Bibi Neema Abson amesema ushiriki mdogo wa makampuni ya Tanzania katika sekta ya mafuta na gesi umetokana na mitaji na uelewa mdogo juu ya sekta hiyo na kusisitiza serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuweka sera ya gesi inatoa kipaumbele cha ushiriki wa makampuni ya kitanzania pamoja na kutoa elimu kwa watanzania. 
Sekta ya mafuta na gesi kwa makampuni ya ndani, mkurugenzi mkuu wa taasisi ya sekta binafsi Bw. Godfrey Simbeye amesema idadi kubwa ya watanzania hawana mitaji ya kutosha na mabenki yaliyopo hayanauwezo wa kutoa mikopo inayokidhi mahitaji ya viwango vya kimataifa vinavyohitajika katika sekta ya mafuta na gesi.
Kwa upande wake makamu wa rais, sera na mambo ya ushirikiano wa kampuni ya uchimbaji gesi ya BG Tanzania Bwana John Ulanga amesema changamoto zinazoyakabili makampuni ya kitanzania ni kufikia viwango vya kimataifa ili kuweza kuzitumia fursa za utoaji huduma na ajira zinazopatikana katika sekta ya mafuta na ges

Post a Comment

 
Top