Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Arfi amesema kama kuna mtu anayekijua vizuri Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ni yeye na wanaombeza kuwa hajafanya kitu katika Jimbo lake la Mpanda Mjini waendelee kumbeza.
ARFI alisema kwa muda mrefu alikuwa kimya licha maneno mengi yaliyosema na Wanachama na Wapenzi wa CHADEMA juu yake , lakini akihitajika kumwaga Mboga ili watanzania kujua udhaifu wa CHADEMA atafanya hivyo.
Arfi aliyasema hayo mjini Mpanda katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashaulili ambapo alitumia nafasi hiyo kuwambia Wananchi wa Mpanda kuwa Uanachama wake ndani ya Chadema utakoma mara tu baada ya kuvunjwa kwa Bunge huku akiweka wazi kuwa hana Mpango wa kugombea Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama chochote cha Siasa.
Post a Comment