0
WATU wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wavamia na kujeruhi na kisha kupora mali mbalimbali baada ya kuweka kizuizi cha mawe/magogo katika barabara ya mbalizi/mkwajuni.

tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo Julai 9,2015 majira ya saa 02:00 huko eneo la Msitu wa Mlima Msangamwelu, Kijiji cha Mjele, Kata ya Mshewe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoa wa Mbeya baada ya watu wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa majambazi kuliwekea vizuizi gari lenye namba za usajili SM 3496 aina ya Toyota Land Cruiser mali ya Hospitali ya Mwambani Chunya lililokuwa likiendeshwa na dereva Loved Mwandongo (53) mkazi wa Mkwajuni.

Gari hiyo ilikuwa imebeba mapadri watatu na mapadri watatu wanafunzi ambao ni 1. Furaha Henjewele (36) Padri mwanafunzi, mkazi wa Mbeya alipigwa fimbo kichwani na kukatwa panga mkono wa kulia 2. Padri Gasper Mwashimwanga (37) mkazi wa mpuguso Tukuyu alipigwa fimbo mwilini.

Mtu wa tatu ni Henry Mwalyanga (33) Padri mwanafunzi, mkazi wa Mbeya alipigwa fimbo mwilini 4. Eliakim kasegila (27) Padri mwanafunzi, mkazi wa Peramiho alijeruhiwa mwilini 5. Padri Bonifasi Cchalo (46) mkazi wa Mwanjelwa alijeruhiwa kwa fimbo mwilini 6. Exavery Mwafumbo (28) padri Mwanafunzi, mkazi wa Mwanjelwa na 7. Dereva mwenyewe Loved Mwandongo (53) alipigwa fimbo mwilini.

Aidha katika tukio hilo wahanga hao ambao walikuwa wanakwenda Galula kuhudhuria sherehe ya upadrisho, waliporwa pesa taslimu ambazo bado kufahamika kiasi gani, mabegi ya nguo mbalimbali, zawadi za waumini, simu za mikononi pamoja na majoho. Wahanga wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa.

Msako mkali unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika tukio hili ili wakamatwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Imetolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya AHMED MSANGI

Post a Comment

 
Top