0

Siri nzito zilizovuja kutoka Team Lowasa hizi hapa

Wadau, amani iwe kwenu.

Wakati CCM wakianza vikao vya ndani vya mchujo wa wagombea ili kumpata mtu mmoja tu ambaye atapeperusha Bendera ya Chama kwenye kinyang'anyiro cha Urais, hali ndani ya Team Lowasa inazidi kuwa mbaya. Kwa sasa hali imekuwa kama wale waliokuwa wanajenga Mnara wa Babeli. Yaani full kujichanganya na mambo yao kwa sasa ni nje nje. Nimefanikiwa kunyaka siri nzito kadhaa za timu hiyo. Miongoni mwa siri hizo zilizovuja kutoka kwenye kambi hiyo ni hizi zifuatazo;

1. Rostam Aziz kukabidhiwa Kinyerezi 1,2 na 3 huku Nazir Karamagi kupewa Bandari ya Dar es salaam ikiwa Lowasa atashinda

Lowasa ameingia makubaliano na Rostam na Karamagi ya namna ya kurejesha gharama wanazotumia kumfadhili mwanasiasa huyo. Mtakumbuka kuwa Nazir na Rostam ndio wafadhili wakuu wa Lowasa na ndio wanaohusika kutoa kiasi kikubwa cha fedha zinazotumika katika harakati za kwenda Magogoni. Mpaka sasa, Rostam ametumia zaidi ya shilingi bilioni 30 huku Karamagi akitumia bilioni 12. Fedha nyingine Lowasa anazipata kutoka kwa watu wengine ambao soon watawekwa hadharani.

Ili kurejesha gharama hizo na nyingine zitakazokuja, Lowasa ameafikiana na wafadhili hao kama ifuatavyo. Rostam Aziz atapewa mitambo ya kufua umeme iliyopo Kinyerezi Dar es Salaam ambayo ni Kinyerezi 1,2 na 3. Aidha, Karamagi atapewa Bandari ya Dar es Salaam ambapo kupitia kampuni yake ya kupakua na kupakia makontena ya TICTS, wataendesha Bandari hiyo. Watatumia kigezo cha serikali kutojihusisha na masuala ya kibiashara. Rostam na Karamagi watapewa deal hilo ambalo Lowasa atasaini mkataba wa miaka 20. Kwa maana nyingine, Rostam atazalisha umeme kwa miaka 20 na Karamagi atasimamia bandari kwa miaka 20. Wanaamini kuwa ndani ya miaka hiyo, watakuwa wamerejesha gharama walizotumia na kupata faida kubwa. Katika kujipanga zaidi, Rostam na Karamagi wamekubaliana kuwa warejeshe gharama hizo ndani ya miaka 5 ya awali ya utawala wa Lowasa na kwamba miaka mingine 15 ni ya kutengeneza faida.

2. Team Lowasa wakutana Perugina Hotel na kuazimia kuanzisha vuguvugu la kutokuwa na imani na Mwenyekiti ndani ya CC.

Edward Lowasa na watu wake wa karibu walifanya kikao jana usiku kwenye Hoteli ya Perugina iliyopo karibu na Uwanja wa Ndege, kando ya barabara ya kuelekea Area C. Katika kikao hicho, wamekubaliana mambo mengi. Ila kwa faida ya wasomaji, hoja kubwa waliyokubaliana ni kuanzisha vuguvugu la kutokuwa na imani na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Kwamba, baada ya ule mpango wa kuhoji uhalali wa kukatwa jina la Lowasa kuumbuka ambapo mpango huo ulipangwa kuongozwa la Emannuel Nchimbi, kwa sasa wanajipanga jinsi ya kuanzisha kumpinga Mwenyekiti ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Watatumia mpango ule ule kama wa awali ambapo makada wale kama Emannuel Nchimbi, Sadifa Juma, Jerry Slaa na Sophia Simba mmoja wao atasimama na kuanzisha hoja ya kutokuwa na imani na Mwenyekiti.

Hoja watakayosimamia ni kauli aliyotoa Mwenyekiti wao hivi karibuni huko Tanga wakati wa maadhimisho ya Jubilee ya miaka 125 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosis ya Kaskazini Mashariki ambapo alisisitiza wananchi tusiwape mwanya wanasiasa wenye dhamira ovu ya kutumia fedha kusaka madaraka. Katika maadhimisho hayo, Rais Kikwete pia aliwaomba viongozi wa dini wakemee watu wanaokiuka maadili na misingi ya dini ambao wanatumia fedha kutaka madaraka.

Pia Team Lowasa wamechukizwa na kauli aliyotoa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kuwa hakuna nafasi ya kukata Rufaa kwa wale watakaoenguliwa kwa vile muda huo haupo na hakuna kanuni inayotoa nafasi hiyo. Ka vigezo hivyo viwili, Team Lowasa wanaona kuwa Mwenyekiti na viongozi wengine wana agenda ya siri dhidi ya mgombea wao na hivyo ni vema wakaanzisha mchakato wa kutokuwa na imani naye.

3. Lowasa akiondoka CCM ataondoka na wabunge 40.

Endapo Lowasa atakatwa, msimamo wake mpaka sasa ni kwamba hatahama chama na badala yake ataendelea kuwa mwanachama wa CCM. Hata hivyo, wafadhili wake na baadhi ya wanasiasa walio karibu naye wanaendelea kumshinikiza ili aondoke. Miongoni mwa wanaosimamia mkakati wa kuondoka ni pamoja na mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola. Kwamba haina maana ya kuendelea kubaki ndani ya CCM kwa vile wamepoteza muda mwingi na fedha nyingi. Kwa hali hiyo wanaendelea na majadiliano ili kumshawishi Lowasa akubali kuwa endapo jina lake litakatwa, wahame CCM na kujiunga na ACT na kwamba Kangi Lugola amemhakikishia Lowasa kuwa anayo majina ya wabunge 40 ambao wapo tayari kuhamia huko ikiwa Lowasa atahamia.

4. Aloyce Tandewa awafukuza vijana 25 na Mganga Mmoja Nam Hotel

Mlinzi Mkuu wa Lowasa, Aloyce Tendewa amewafukuza vijana 25 waliosafirishwa kutoka Arusha kwa ajili ya kufanya vurugu Dodoma endapo jina la Lowasa litakatwa. Pia mganga mmoja miongoni mwa wale waganga 10 waliopo hotelini hapo ambao wana lengo la kuhakikisha Lowasa anakuwa mgombea wa CCM amefukuzwa. Sababu zilizotolewa na Tendewa ni kwamba vijana hao na mganga huyo wamekuwa wakivujisha siri za ndani ya hoteli hiyo. Kwamba, vijana hao wamepekuliwa kwenye simu zao na wakagundua kuwa walikuwa wanafanya mawasiliano na watu ambao wanahisi ni wabaya wao. Vijana hao wamesindikizwa leo chini ya ulinzi na wamerejeshwa Arusha kwa basi maalum la kukodi.
Ila huku ni kupakana matope sijui
Chanzo Jamii Forum

Post a Comment

 
Top